Jalada kesi Malinzi wenzake laludishwa kwa DPP...soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam
TAKUKURU wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  kuwa hadi Jumatatu jalada la kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la  Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi(57) na wenzake litakuwa limerejeshwa  kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hatua hiyo ni kufuatia upande wao kukamilisha upelelezi katika kesi hiyo. Mbali na Malinzi wengine wanakabiliwa na kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa  Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Mwanga(27).
Jamali Malinzi katikati akiwa na wenzake katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu
Leo wakili wa Takukuru Leonard Swai amedai kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba kuwa wao kama Takukuru wamekwisha kamilisha upelelezi kwenye kesi hiyo na hadi Jumatatu litakuwa  limetua kwa DPP.

Swai amedai awali jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa DPP, alilipitia na kurirejesha Takukuru kwa maelekezo ambayo wameyafanyia kazi.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 8,2018.

Washtakiwa hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29,2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418. 


Katika kesi hiyo, Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 huku wenzake wakikabiliwa na makosa yasiyozidi manne.

Wakati kesi hiyo ikitajwa washtakuwa wote walikuwapo mahakamani na wanatetewa na mawakili Nehemia Nkoko, Dokinician Rwegoshora na Abraham Senguji.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search