Waziri aagiza waliokula fedha za Tasaf wafikishwe mahakamani...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Mbeya.

UONGOZI wa Mkoa wa Mbeya umeagizwa kufuatilia sh milion 32 
zilizotolewa kimakosa kwa kaya 20 kupitia mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) na watakaoshindwa kurejesha wafikishwe mahakamani.


Waziri George Mkuchika

Agizo hilo limetolea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais   Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika,  baada ya kupata taarifa ya  jumla ya kaya 54 zenye sifa kukosa ruzuku huku fedha nyingi zikilipwa kwa  kaya zisizo na sifa.

"Nasikitishwa na kaya zilizoondolewa kwenye mpango kutochukuliwa hatua zozote. Hili halikubaliki ni lazima fedha zirejeshwe ili zisaidie kaya ambazo hazikuingizwa kwenye mpango," amesema Mkuchika


Katibu Tawala Mkoa, Mariam Mtunguja amesema  katika awamu ya pili  na tatu ya mradi mkoa  huo uliopokea zaidi ya sh bilioni 9 kwa ajili ya
kutekeleza miradi  379.

Amesema hadi sasa tangu mpango huo uanze  mkoa umetumia zaidi ya
sh bilioni 26.7 katika awamu 15  na jumla ya kaya 42,000 zimenufaika, kati ya fedha hizo sh bilioni 3 zimetumika katika ufuatiliaji.

Mratibu Tasaf wa jiji hilo, Emmanuel Kimbe amesema kuna  miradi 77 ikiwemo  ya afya, elimu, miundombinu na makundi maalumu yenye thamani ya sh bilioni  2.8

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search