Kambi ya upinzani yasusa Bungeni....soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WIZARA ya Katiba na Sheria kambi rasmi ya upinzani bungeni
imesusa kusoma maoni ya upinzani kuhusu mswada wa marekebisho ya sheria mbali
mbali nchini.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge
kumzuia Ally Salehe kusomwa kwa baadhi ya maneno yaliyomo katika maoni hayo.
Salehe alikuwa akisoma maoni hayo leo kwa niaba ya Msemaji wa
Wizara hiyo Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya
kushambuliwa kwa risasi Novemba 7 mwaka jana.
Maneno yaliyozuiwa kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya
uhalifu nchini, likiwemo la kushambuliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu
Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Tundu Lissu.
Salehe alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya nne
alizuiwa na Chenge akimtaka asubiri ambapo baadae alimueleza kuwa lugha
iliyotumika katika ukurasa wa kwanza na wa pili wa hotuba hiyo si ya kibunge.
Baada ya kauli hiyo, Salehe amesema upinzani unaiamini na
unaisimamia hotuba hiyo kwa kuwa wabunge wote wanayo nakala yake na kuomba
kuiwasilisha na kurejea kuketi.
No comments:
Post a Comment