Kunguni wazua taharuki ndani ya ndege...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
WAZIRI wa uchukuzi  nchini Ghana, Cecelia Dapaah amelitahadharisha shirika la ndege la Uingereza, British Airways, kwamba huenda likaadhibiwa vikali.
Hii ni baada ya kunguni kugunduliwa kuwepo katika baadhi ya ndege za shirika hilo na wahudumu kuzua taharuki walipokurupuka nje badala ya kuwaelekeza wasafiri kuingia ndani ya ndege hiyo.

Gazeti moja la Uingereza wiki hii liliripoti kwamba ndege moja ya BA ilizuiwa kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London kuelekea Accra baada ya kunguni kugunduliwa wakitambaa kwenye viti vya ndege hiyo.
Gazeti la The Sun lilichapisha habari kuwa wahudumu wa ndani ya ndege hiyo walipigwa na butwaa walipowaona kunguni wengi tu ndani ya ndege na kulazimu kuahirishwa kwa safari yao.
Shirika hilo la ndege limejitetea likisema tukio hilo sio la kawaida na kwamba ndege hiyo haikuruhusiwa kuondoka uwanja wa ndege na haikufika mjini Accra.
Shirika hilo limesema limejitolea kutoa huduma ya hali ya juu kwa abiria wake. Shirikala BA limehudumu nchini Ghana kwa miaka 80.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari mapema leo, shirika hilo la British Airways limesema kuwa limewatuma wataalamu wa kukabili ueneaji wa wadudu hao kulishughulikia suala hilo kikamilifu.
Licha ya maelezo hayo, waziri anayesimamia usalama wa anga nchini Ghana Bi Dapaah ameionya British Airways kuwa huenda hatua za kinadhamu zikachukuliwa dhidi yake iwapo tukio hilo halitakabiliwa haraka.
Tukio hilo la aibu ndilo la hivi punde zaidi kuikumba British Airways ambaye kwa mtazamo wa wengi imeathirika vibaya kutokana na kudorora kwa viwango vyake vya huduma kwa wateja.
Shirika hilo la ndege la Uingereza British Airways huwa halina ushindani mkali katika safari kati ya mji mkuu wa Ghana Accra na London.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search