Pogba ataka kulipwa zaidi ya Sanchez Man Utd....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa
MCHEZAJI wa Manchester United, Paul Pogba sasa anataka kulipwa mshahara mara mbili ya anaoupokea sasa wa paundi laki mbili kwa wiki na klabu yake hiyo. 

Hatua yake hiyo ni kutaka mshahara wake ufanane au uzidi wa  mchezaji mpya wa timu hiyo Alexis Sanchez atakayekuwa akilipwa paund laki nne na nusu kwa wiki.


Paul Pogba


Wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola amesema kwa sasa thamani ya malipo ya mshahara wa  mchezaji mwenye ubora kama wa Pogba ambaye ni raia wa Ufaransa umeongezeka maradufu katika dirisha la usajili na kwamba Pogba anastahili kulipwa zaidi ya paundi laki nne kwa wiki.

Kiungo huyo mbunifu aliyenunuliwa mwaka jana kwa paundi milioni 89 kutoka klabu ya Juventus ya Italia amebakisha miaka mitatu ya mkataba wake wa kuichezea timu ya Man Utd.

Wakala Raiola amesema mkufunzi wa Manchester united, Jose Mourinho anajua umuhimu wa mchezaji huyo na ili ambakishe klabuni hapo hana budi kumuongezea mkataba wa muda mrefu na kumlipa mshahara mnono wa kumfanya Pogba awe ni mwenye furaha




About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search