Vigogo watatu Maliasili wapandishwa kizimbani ....soma habari kamili na matukio 360...#share
Na Mwandishi
Wetu,Dar es Salaam
WAFANYAKAZI watatu
wa Wizara ya Maliasili na Utalii leo wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya dola 32,599.
Wakili wa Serikali
kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini(Takukuru) Leonard Swai,
amewataja washtakiwa hao ni, Ofisa Muhifadhi anayehusika na uwindaji wa
matumizi endelevu ya wanyamapori Rajabu Hochi, Ofisa wa Muhifadhi mwenye wajibu
wa kukusanya wa mapato ya uwindaji , Mohamed Madehele na Isaac Maji.
Mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa, washtakiwa wakiwa watumishi kitengo
cha Wanyamapori, walitenda makosa hayo katika makao makuu ya wizara hiyo.
Akisoma hati ya
mashtaka wakili wa serikali Pendo Temu amedai,kati ya Januari 12 na Desemba 31,
mwaka 2008, makao makuu ya wizara hiyo, Hochi na Madehele wakiwa watumishi wa
wizara hiyo, wakiwa na wajibu wa kukusanya mapato yanayotokana na uwindaji
walitumia madaraka yao vibaya kwa kuzidisha wanyama pori kwa Kampuni ya
Uwindaji ya Northern Hunting Enterprises (Tanzania) kinyume cha sheria na hivyo
kuiwezesha kampuni hiyo kupata faida ya USD 250 isivyo halali.
Pia Hochi na
Madehele, wanadaiwa kati ya Agosti 11 na Desemba 31, mwaka 2011, makao makuu ya
wizara hiyo,waliiwezesha kampuni hiyo kujipatia dola za Marekani 250 isivyo
halali.Aidha, Hochi na Madehele, wanadaiwa, kati ya Septemba 5 na Desemba
31,mwaka 2010, walishindwa kukusanya faini ya dola za Marekani 15,630 kutoka
katika kampuni hiyo.
Washtakiwa Hochi na Madehele,wanadaiwa kushindwa kukusanya faini ya dola za Marekani 250 kutoka kampuni ya uwindaji ya Hunting Enterprises (Tanzania), kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment