Weah kuapishwa leo Wenger, Drogba, Etoo kushuhudia...soma habari kamili na matukio360...#share

Na mashirika ya kimataifa

RAIA wa Liberia wamekesha kuamkia leo katika uwanja mkuu wa taifa katika jiji la Monrovia kusheherekea uapishwaji wa rais mteule wa nchi hiyo, George Weah huku kocha Aserne Wenger, mchezaji Samuel Etoo na Didier Drogba ni miongoni mwa watakaoshuhudia kuapishwa kwake.

Weah aliyeshinda duru mbili za uchaguzi anaapishwa rasmi leo kuchukua nafasi ya mtangulizi wake, Ellen Jonson Sirleaf ambaye alikuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.

Rais mteule wa Liberia, George Weah

Weah ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa Dunia wa shirikisho la soka Duniani(FIFA) alimshinda makamo wa rais wa nchi hiyo, Joseph Boakai.

Alishinda katika uchaguzi  baada ya kushinda katika wilaya 12 miongoni mwa 15 zilizomo katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.

Weah ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuwashukuru watu wote waliompigia kura akisema mipango yake ni kuleta ukombozi kwa nchi nzima.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya AC Milan ya Italia, anakuwa rais wa 25 wa nchi hiyo ambapo aliyekuwa makamu wa rais kwa miaka 12 iliyopita, Joseph Boakai, alipata ushindi katika wilaya mbili tu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search