Mashabiki wamzomea Neymar ....soma habari kamili na matukio 360...#share
Na mashirika ya kimataifa
MASHABIKI wa timu ya Paris St-Germain wamemzomea Star wa timu hiyo Neymar baada ya kumnyima Edinson Cavani fursa ya kupiga penati ili awe mchezaji aliyeifungia klabu hiyo mabao mengi katika mechi dhidi ya Dijon.
Cavani Na Neymar wakigombea kupiga penati
Bao la kipindi cha kwanza la Cavani lilimfanya kuwa sawa kwa magoli na mshambuliaji wa zamani, Zlatan Ibrahimovic akiwa na magoli 156 katika mashindano yote aliyochezea PSG.
Wenyeji hao waliongoza kwa 4-0 katika kipindi cha kwanza na Neymar alikuwa tayari amekamilisha hat-trick kabla ya PSG kupata penalti.
Hata hivyo raia huyo wa Brazil aliamua kupiga mkwaju huo wa penalti badala ya kumwachia Cavani, hatua iliomfanya Neymar kuzomewa na mashabiki wa timu hiyo , lakini kocha Unai Emery alimtetea mchezaji huyo baada ya mechi hiyo.
Nadhani Neymar alipiga mkwaju huo wa penalti kwa sababu ilikuwa siku nzuri kwake'', alisema Emery.
''Tunafurahia. Lakini kutakuwa na fursa nyingi kwa Cavani kufunga mabao zaidi''.
Beki wa PSG Thomas Meunier aliitaja hatua hiyo ya Neymar kuwa aibu lakini akaongezea kuwa ni Neymar aliyepewa jukumu la kupiga penalti.
''Angempatia mpira ingekuwa ishara nzuri ya fair Play'', alisema.
''Aliifanyia kazi kubwa timu yetu na swala la kuzomewa na mashabiki , kwa kweli hakuipiga vizuri. Nadhani wachezaji wengi wangefanyiwa hivyo''.
PSG inaongoza kwa pointi 11 kutoka kwa wapinzani wake wa karibu Lyon baada ya mechi 21.
Viongozi hao wa ligi wameshinda mechi nane zilizopita na michuano ya kuwania mataji, wakiwa wamefunga mabao 31 na kufungwa sita pekee.
Dijon ambao wako katika nafasi ya 11 katika jedwali hawajashinda hata mechi moja katika mechi nne walizocheza.
No comments:
Post a Comment