Morocco yazindua kampeni kuandaa mashindano ya soka ya dunia...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
Morocco imezindua kampeni yake ya kuandaa mashindano ya kombe la dunia ya 2026 mjini Casablanca.
Taifa hilo la Afrika kaskazini ambalo limewasilisha ombi lake la tano kuandaa fainali hizo , linakabiliwa na ushindani mkali kutoka ombi la pamoja linaloshirikisha Canada, Mexico na Marekani.
Mwenyekiti wa ombi hilo Moulay hafid Elalamy amesema kuwa Morocco itaonyesha mchezo mzuri zaidi, katika kombe hilo la dunia.
Uamuzi wa ni nani atakayeandaa kombe hilo utafanywa Juni 13 mkesha wa kombe la dunia la mwaka 2018 mjini Moscow.
''Tunaahidi kuonyesha mchuano mzuri na kusheherekea thamani ya Umoja na amani'', aliongezea Elalamy.
''Maandalizi ya kombe la dunia nchini Morocco yataleta ufanisi wa kibiashara na kuacha historia kubwa, na iwapo tutashinda heshima ya kuandaa dimba hilo tunaamini kwamba mshindi atakuwa soka, vijana wa taifa letu ,Afrika na dunia nzima kwa jumla''.
Taifa hilo la Afrika kaskazini limefeli katika maombi yake manne la mwaka 1994, 1998, 2006 na 2010.
Mwaka 2010, michuano ya kombe la dunia iliandaliwa na Afrika Kusini ikiwa ni historia kwa bara la Afrika
Morocco inataka kubadili hayo yote na imemteua Elalamy, waziri wa serikali, kuongoza ombi hilo huku aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka Afrika Hicham El Amrani akiwa afisa mkuu mtendaji.
No comments:
Post a Comment