Rais Museveni awaponda waafrika amsifu Trump...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema anampenda rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na kuongea ukweli na kwamba waafrika ni dhaifu.
Ameeleza msimamo wake huo jana katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala.
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema anampenda rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na kuongea ukweli na kwamba waafrika ni dhaifu.
Ameeleza msimamo wake huo jana katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala.
Museveni alisema Marekani ina rais mzuri
''Ninampenda Trump kwa sababu anasema ukweli mtupu, waafrika wanatakiwa kusuluhisha matatizo yao wenyewe, waafrika ni dhaifu sana,'' amesema Museveni.
Pongezi hizo za Museven kwa Trump zinakuja saa chache tuu baada ya balozi wa Uganda nchini Marekani, Deborah Malac kumkosoa Trump. Akisoma ''Kauli zake zinachukiza na kukera sana."
Maoni hayo ya rais Museveni ni tofauti na viongozi wengi wanaochukizwa na kauli za Trump.
Mapema mwezi huu Trump alidaiwa kutoa kauli za kejeli juu ya nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji.
Trump alikataa kuwa ametoa kauli hizo za kejeli lakini seneta mmoja aliyehudhuria mkutano huo alisema kuwa Trump alitamka maneno ya kejeli na matusi kwa nchi kama Haiti, elsalvador na nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa gazeti la New York times, mwaka jana Trump alisema kuwa watu wote wanaotoka Haiti wana ukimwi, na wananigeria wakiruhusiwa kuingia marekani basi watakataa kurudi kwao. Hata hicho Ikulu ya White House ilikanusha madai ya kauli hizo.
No comments:
Post a Comment