Mratibu akamatwa mbele ya Waziri...soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Ukerewe
MRATIBU wa mradi wa mabwawa ya samaki Namagondo wilayani Ukerewe mkoani Mwanza aliyefahamika kwa jina la Jackson amewekwa chini ya ulinzi kwa kuidanganya serikali na ubadhilifu wa mali za umma.

Mratibu bwawa la samaki Namagondo ,Jackson akiwa chini ya ulinzi wa polisi

Hatua huyo inafuatia baada ya naibu waziri ofisi ya makamu wa rais Muungano na mazingira Kangi Lugola  kukagua mradi huo  na kubaini hakuna kilichofanyika na fedha milion 317 hazieleweki zimefanya kitu gani kwenye mradi huo.

Pia hatua huyo imefikiwa baada ya ukaguzi uliofanyika na wakaguzi wa wizara hiyo mwaka jana na kuibua uozo huo.

" Nimethibitisha yale yote yaliyosemwa na wakaguzi kuwa ni kweli. Huyu ndugu Jackson akamatwe na kufikishwa mahakamani," amesema Lugola 

Waziri Lugola akizungumza na baadhi ya wananchi wa Ukerewe


Waziri Lugola aliyevaa traki suti ya rangi ya bluu akienda kukagua bwawa la samaki la Namagondo wilayani Ukerewe 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search