Rais Mnangagwa ampa ofa Mugabe....soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
RAIS wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amesema atampa malipo mazuri ya kustaafu rais aliyeng`olewa madarakani, Robert Mugabe na mkewe.

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa
Amesema Mugabe ataendelea kupokea mshahara wake na mafao mengine kama kawaida ikiwemo kusafiri katika kiwango cha kwanza kwenye ndege (first class), pamoja na kusafiri kwa gharama ya serikali.
Lakini Rais Mnangagwa amesema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na asiyeweza kushtakiwa.
Na Amesema kuwa Zimbabwe itajiunga tena hivi karibuni na mataifa ya jumuia ya madola.
'Hatujampa kinga mtu yoyote isipokua ambacho nimeahidi kwa rais aliyetangulia na baba wa taifa letu, rais Robert Mugabe ni kwamba tunampatia mafao na mshahara wake kama alivyokua akipata awali, usafiri, ofisi, ulinzi, na serikali yangu itamuwezesha kuenda Singapore kwenye matibabu, na vyote hivi mke wake pia ataviapata''.
Mnangagwa amesema pia serikali yake mpya inafanya jitahada kubwa za kupambana na rushwa.
'' Msimamo wangu ni kwamba rushwa haiwezi kuvumiliwa hata kidogo, hatuwezi kabisa kuvumilia jambo kama hili , na kama mnafatilia mambo yanayotokea Zimbabwe kwa sasa , watu wengi wenye wadhifa mkubwa wamefikishwa mbele ya mahakama, na ni ndani ya miezi miwili tu tayari tunawashughulikia watu wenye makossa ya rushwa''.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search