Makonda awapa miezi tisa wauza magari....soma habari kamili na matukio 360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaongezea muda wa miezi tisa wauza magari jijini Dar es salaam na kusema baada ya hapo asiwepo mtu wa kuomba kuongezwa muda mwingine.
Paul Makonda
Hatua hiyo inafuatia wafanyabiashara hao kuomba kuongezewa muda wa miezi tisa ili waweze kuhamisha vitu vyao na wanafurahishwa na hatua ya serikali kuhamisha showroom zote kwenye eneo moja Kigamboni na wako tayari kuhama kwa kuwa wataongeza ufanisi, idadi ya wateja na kuleta ushindani mzuri wa kibiashara
Makonda ametoa uamuzi huo katika mkutano wake na wamiliki wa showroom na kuwa ifikapo Oktoba mosi showroom zote ziwe zimehamiha Kigamboni.
Mkuu wa mkoa huyo amesema tayari serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu yote muhimu ikiwemo Barabara, Maji, Umeme, Kituo cha Polisi, Madaraja ili wafanyabiashara wafanye biashara kwenye mazingira bora.
"Faida za uwepo wa showroom kwenye eneo moja ni kupunguza usumbufu kwa wananchi, Mipango miji, ulipaji kodi, kudhibiti wizi wa magari pamoja kuifanya Dar es salaam kuwa soko kubwa la magari Afrika," amesema
Amesema ndani ya eneo hilo zitapatikana ofisi zote zinazohusiana na biashara za magari ikiwemo TRA, TPA, Bank, Gereji, Sheli, Vituo vya polisi na Fire (ones stop center.)
Wafanyabiashara hao wamepewa ofa ya kufanya biashara kwa miaka mitatu kwenye eneo hilo pasipokulipa kodi pamoja na fursa ya kuunganishwa na wauzaji wakubwa wa magari kutoka Dubai kwa ajili ya kufanya ubia.

No comments:
Post a Comment