Rugemarila atoa ya moyoni mahakamani...soma habari kamili na matukio360...#share



Na mwandishi wetu, Dar es salaam
JAMES Rugemarila anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, amewataja Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong kuwa ndiyo wezi wa fedha za Escrow.
James Rugemarila akiingia kwenye gari la askari magereza
Wezi hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine
"Mwizi ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong ambao wameisababishia serikali hasara ya trilioni 37, pia nimewapelekea Takukuru washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao," amesema. Rugemarila
Pia Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai trillion 16. 
Wakili Swai amekiri kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.
Pia Rugemarila ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi nchini India kwani anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9 sasa huku mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ameiambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.
Kutokana na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search