Kanuni kutozungumza siasa,kufanya biashara katika mabasi yaanza kazi....soma habari kamili na matukio360..#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Usimamizi wa
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imewataka wadau wa usafirishaji
wakiwemo wamiliki wa mabasi, madereva na abiria kuzingatia kanuni mpya za
leseni ya usafirishaji ikiwemo kutozungumza siasa,dini na kufanya biashara ndani ya basi.
Mkurugenzi wa barabara wa Sumatra Johansen Kahatano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa barabara za Sumatra, Johansen Kahatono alipokutana na wadau hao kuwapa elimu ya kanuni hizo.
“Nachowataka ni kwamba
wadau wa usafirishaji wanatakiwa kuzingatia kanuni hizi kwani zina manufaa
kwao,” amesema Kahatano.
Amesema katika kanuni hizo kuna mabadiliko ambayo yamefanyika
kwenye leseni za usafirishaji wa mizigo huku zikitengenezwa mpya kwa upande wa
usafirishaji wa abairia.
Kahatano amesema kanuni zinawataka abiria kutozungumza
masuala ya siasa way a dini ndani ya mabasi wakati wakisafiri.
Ameongeza zitamtaka abiria kuweka wazi mizigo waliyonayo ili
iwe rahisi kubaini kama wamebeba mizigo haramu.
Hata hivyo mjumbe wa halmashauri kuu ya Taboa taifa Mwesigwa
Kazaula aliomba serikali kuendelea kuboresha mazingira katika sekta hiyo ya usafirishaji kwani ndiyo njia pekee inayowaingizia kipato.
No comments:
Post a Comment