Serikali sasa kutoa chanjo ya saratani nchini...soma habari kamili na matukio 360..#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


SERIKALI inatarajia kutoa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto na kwamba kila mwaka wagonjwa wapya 50,000 hupata saratani na milion nane hufariki


 Daktari bingwa wa magonjwa Saratani, Kitengo cha Bima (ORCI). Dk. Mark Mseti akitoa semina kwa wahariri juu ya magonjwa ya saratani ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya saratani duniani Febuari 4 . semina hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam Taasisi ya Ocean Road

Hayoyamebainishwa Dar es Salaam leo, wakati wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya saratani Duniani Febuari 4 kila mwaka.


Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na  Saratani ORCI, Dk. Crispin Kahesa amesema chanjo hiyo itaanza kutolewa bure kwa wasichana kuanzia darasa la nne kwa dozi mbili kila baada ya miezi sita nchini kote.


"Bado Saratani ya shingo ya Kizazi ni tatizo kubwa... Idadi ni kubwa imezidi asilimia 36 na inawaathiri zaidi wanawake, "amesema.


Amesema  mbali na kutolewa chanjo saratani hiyo inatibika endapo ikiwahiwa katika hatua ya kwanza.



"Serikali mwaka huu imeamua kwa watoto wetu wote watapewa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi,"amesema.


Amesema chanjo hiyo haina mahusiano na mfumo wa kizazi bali inazuia virusi vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi na kutibu kizazi.


Amefafanua magonjwa ya saratani hayachagui umri wala jinsia na kwamba mwaka  2000  kulikuwa na wagonjwa wapya milioni 10 ambapo sasa wamefikia milioni 14 huku milioni nane wakifariki kila mwaka.


Kwa upande wake Daktari bingwa Magonjwa ya Saratani, Kitengo cha Bima (ORCI), Dk.Mark Mseti amesema  matibabu ya saratani hutegemea hatua ya saratani, hali ya mgonjwa  na utayari wa mgonjwa kupata tiba.


Amefafanua wagonjwa wa saratani hupata maumivu makali na kwamba huwafanyia upasuaji wa uvimbe au kupunguza ukubwa wa uvimbe na kuwawekea mionzi ili kuuwa seli  zisisambae.


Ameongeza kuwa tiba nyingine ni mgonjwa kupewa kemikali yenye kuuwa seli na dawa za kuwezesha saratani isisambae.


"Wengine huhitaji aina moja ya tiba lakini mara nyingi wagonjwa hupata aina mbili ya tiba,"amesema.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search