Hizi hapa ahadi za mgombea ubunge CUF Kinondoni..soma habari kamili na matukio360...#share
Na Abraham Ntambara,
Dar es Salaam
MGOMBEA ubunge wa jimbo
la Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi CUF Rajab Juma, ameeleza vipaumbele
vinne ambavyo atavisimamia atakapopewa ridhaa ya kiti hicho.
Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CUF Abdul Kambaya akimnadi Mgombea wa jimbo la Kinondoni Rajab Juma jijini Dar es Salaam.
Akiomba kura kwa wakazi
wa Kijitonyama katika viwanja vya Alimaua jijini Dar es Salaam, Juma alitaja
vipaumbele hivyo kuwa ni elimu, afya, ajira na miundombinu.
“Kipaumbele cha kwanza
ni elimu na nitakachofanya katika elimu utakapoletwa mswada wa elimu nitachangia
hoja kutaka serikali iongeze mishahara kwa walimu ili wajikite zaidi katika
kufundisha wanafunzi badala ya kufanya biashara ya kuuza biskuti shuleni, hii
itaongeza ufaulu kwa wanafunzi,” alisema.
Afya, alisema baada ya
mtu kuwa na elimu anatakiwa kuwa na afya, hivyo atahakikisha kunakuwa na mfuko
maalum wa matibabu ambao utawaanezi wazazi wajawazito, watoto wachanga na wazee
ili kupata matibabu kwa gharama nafuu.
Ajira, alisema
akichaguliwa atasimama imara katika kuanzisha na kusimamia miradi midogomidogo
ya wafanyabiashara wadogo kama vile bodaboda na kuwaunganisha kuweza kusajili
katika vikundi ili wajitafutie riziki za haralina kwa ajili ya kujikimu
kimaisha, kusaidia wazazi na kusomesha watoto.
Miundombinu, alisema maeneo
mengi ya Kinondoni yameathirika kijografia na hayako salama pale mvua
zinaponyesha kwani kila mahali panakuwa pamefurika maji hivyo atahakikisha
miundombinu kama ya barabara inaboreshwa.
No comments:
Post a Comment