Serikali yapiga 'stop' utoaji hati za kusafiria, taasisi zapewa siku mbili...soma habari kamili na matukio360..#share

Na Salha Mohamed, Dar es salaam

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza kusimamisha zoezi la utoaji hati za kusafiria za jumla na kwa makundi hadi hapo utaratibu mpya utakapotolewa

Pia imeagiza taasisi zote, leo na kesho kuhakiki upya vibali vyao vya kufanyia kazi nchini.

Waziri, Dk Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Tamko hilo limetolewa  leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Mwigulu Nchemba wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  na kusema hatua hiyo imekuja baada ya kupokea taarifa ya mateso wanayoyapata vijana wanaosafirishwa kutoka  Tanzania kwenda nje ya nchi kwa kisingizo cha kufanyakazi tofauti.

"Natoa tamko na kuelekeza kwamba nasimamisha utoaji wa hati ya kusafiri 'Passport' za jumla. Vijana wetu  wanapata mikasa  ya kunyanyaswa, kutumikishwa, kuteswa kikatili na wengine kuwekwa rehani kwa masuala ya dawa za kulevya," amesema.

Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema "Tunasimamisha hadi hapo tutakapokuwa tumeweka utaratibu uliorasmi na mzuri kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya nchi husika ambako kutakuwa na mahitaji ya aina hiyo. Mfano mzuri Kenya ilipokuwa inahitaji madaktari walitumia utaratibu uliyo rasmi kuomba madaktari hao. Kwa hiyo huo ndio utakaji wa kundi wa raia walio wengi kwa pamoja."

"Pia nazitaka taasisi zote zilizo na vibali  vya kufanya shughuli zake nchini zihakiki upya kuanzia aleo na kesho itakuwa mwisho na endapo hawatafanya hivyo hatua kali zitafuatwa," amesema

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search