Mahakama yaelezwa Aveva mgonjwa wa figo, amelazwa...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi kusutu leo imeelezwa mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya kughushi  rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na Figo.


Mbali na Aveva mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni makamu wa rais wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' ambaye alikuwepo mahakamani hapo

Mwendesha mashtaka mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameeleza hayo
 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa  na kwamba upelekezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Amedai walishachukua maelezo ya mshtakiwa wa pili na kwamba wanaangalia jinsi ya kupata maelezo ya mshtakiwa wa kwanza ambaye anaumwa kwa sasa.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi February 8,2018  kwa ajili ya kutajwa.

Evans Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha Dola za kimarekani 300,000.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search