Tundu Lissu aishtaki Tanzania kimataifa...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mashirika ya kimataifa
MWANASHERIA mkuu wa chama cha Chadema, Tundu Lissu  ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana
Tundu Lissu
Pia  Lissu ambaye ni mbunge was Singida Mashirika amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba,2 017 unaoendelea.
Aidha, amesema rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi kuzungumzia hadharani kisa cha kushambuliwa kwake.
"Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawakilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," amesema Lissu.
 Lissu amesema amepona na kwamba anashukuru Mungu na wote waliomtakia uponaji wa haraka.i
Katika hatua nyingine mnadhimu huyo mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema  amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali.
Leo nchini Kenya akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani.
Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali. 
Lissu ameyazungumza hayo kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search