UPDATES: Tundu Lissu atoka hospitali kwenda Ulaya...soma habari kamili na matukio360..#share

Na mwandishi wetu

MWANASHERIA mkuu wa chama cha Chadema, Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka hospitali nchini Kenya na kesho anasafiri kwenda barani Ulaya kwa matibabu ya viungo.

Tundu Lissu

Akizungumza na matukio360 Kwa njia ya simu jioni hii, Lissu amesema mapema kesho asubuhi anasafiri kwenda Ulaya.

"Siwezi kusema ni nchi gani barani Ulaya ninayokwenda kwa sababu za kiusalama. Afya yangu imetengemaa ninakwenda  kwa ajili ya matibabu ya viungo," amesema Lissu

Lissu ametibiwa kwa takribani miezi minne nchini Kenya baada ya kupigwa risasi mjini Dodoma Septemba 7, 2017

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search