UVCCM wairushia kombora Chadema....soma habari kamili na matukio360...#share


Na Salha Mohamed, Dar es Salaam 

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) umeifananisha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  kama kamati ya harusi.

Pia umesema CCM itashinda kwa kushindo katika uchaguzi mdogo wa marudio wa ubunge katika jimbo la Kinondoni na Siha, utakaofanyika Februari 17,2018


Vijana wa Umoja wa CCM,  wakila kiapo cha maadili ndani ya chama leo jijini Dar es Salaam  katika kongamano lililoandaliwa na UVCCM, chuo kikuu cha Dar es Salaam

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa UVCCM-Taifa, Kheri James katika kongamano la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo vijana 200 wamejiunga na umoja huo kutoka chuoni hapo. 

James amesema uongozi wa chama hicho unapokea maagizo kutoka kwa mwenyekiti Freeman Mbowe  na kutekeleza huku kukiwa hakuna demokrasia kama ambavyo bwana harusi anapotaka jambo lifanyike kwenye harusi yake na kuwa.


"...Kile si chama nakiita kamati ya harusi kwa sababu, tofauti ya chama na kamati ya harusi ni moja, chama lazima wanachama na viongozi muamue kutokana na mahitaji ya wanachama lakini kamati ya harusi anachokitaka bwana harusi na bibi harusi ndiyo hicho hicho. 

"Huku kwa wenzetu anachokitaka yule jamaa( Mbowe) ndiyo hicho hicho hakuna demokrasia uhuru wa mawazo wala nini....sasa wale si chama cha siasa kile, sisi tumebahatika kuwa kwenye chama cha siasa kinachofuata misingi na demokrasia, "amesema. 

James amefafanua kuwa "Hakuna upinzania mwaka huu...hivi Mbowe ni mpinzani... Lema ni mpinzani... Hakuna mpinzani nchi hii Salum Mwalimu ndiyo kidume aliyetafutwa ili alete ushindani watu wanawacheza shere ...

"Faida tulopata safari hii wametuletea mtu wa kushindwa, kaomba Ubunge kwao visiwani kapigwa, kaja wa Afrika Mashariki kapigwa na Kinondoni atapigwa, "amesema. 

Katika hatua nyingine amewataka vijana nchin kuwa wamoja ili kuwa na mafanikio ya muda mrefu na kutoruhusu vibaraka kuharibu taswira ya nchi.

"Kibaraka anayetumika ndani ya CCM  na wale wanaomtumia hawatabaki salama... Mijadala ya kudhoofisha jitihada zinazofanywa na serikali na kuzungumza lugha hasi bila kutoa njia mbadala kwa serikali na jamii huo ni uharamia katika nchi, "amesema. 

Amesema vijana hao wanapoamua kuikosoa serikali lazima watoe njia mbadala na kwamba watumie elimu yao kulisaidia taifa kuikosoa madhaifu yaliyopo serikali kwa staha ili kusaidia taifa kwani rais anapokea ushauri na kuelekezeka. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search