Vigogo Six Telecoms waendelea kusota rumande...soma habari kamili na matukio 360..#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KESI ya uhujumu uchumi inayowakaili vigogo wa kampuni ya
mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo wakili Dk. Ringo Tenga na wanzake imeahirishwa hadi Januari 26, 2018 kutokana na upelelezi kutokamilika.
Pichani ni Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo hao Watatu wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms, akiwemo Wakili Dk Ringo Tenga na wenzake wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu .
Mbali na Dk. Tenga, washitakiwa
wengine ni Mfanyabiashara Peter Noni, Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
hiyo, Hafidhi Shamte, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na
Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Wakili wa Serikali, Leonard Challo
alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imekuja
kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado unaendelea.
Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo
hadi Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, inadaiwa kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam washitakiwa, walitoza malipo ya simu za kimataifa kwa kiwango cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.
Katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, inadaiwa kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam washitakiwa, walitoza malipo ya simu za kimataifa kwa kiwango cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa katika
tarehe hizo, washtakiwa waliisababishia TCRA hasara ya Dola za Marekani
3,736,861, sawa na Sh bilioni nane.
No comments:
Post a Comment