Wenyeviti serikali ya mtaa wamshtaki mkuu wa wilaya sekretarieti ya maadili...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
WENYYEVITI watatu wa Serikali ya mtaa wa Kimara Baruti, Mavurunza na Makoka wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam leo wamefikisha malalamiko ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya mkuu wa wilaya hiyo, Kisare Makori katika Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Wenyeviti wa serikali ya mtaa wilayani Ubungo wakiwa nje ya ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es salaam leo kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Makori
Wenyeviti hao ni Josephat Mafula mtaa wa Mavurunza, Aloyce Kinyonga mtaa wa Kimara Baruti na Emmanuel Akyoo mtaa wa Makoka.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baaada ya wenyeviti hao kufikisha malalamiko hayo kwa tume wamesema matukio ya matumizi mabaya ya madaraka yamekuwa endelevu .
Mwenyekiti wa Mavurunza, Mafula alisema mkuu huyo wa wilaya amekuwa akiwakamata viongozi wa mitaa na kuwaweka kifungoni bila kutoa sababu yoyote.
Alisema jambo la kusikitisha ni wapinzani pekee ndio wanaokamatwa hata kama hakuna kosa hivyo imani yao ni kupitia tume watapata muafaka.
“Tume yaa maadili ni chombo kinachosimamia maadili ya viongozi hasa wale ambao wanatumia madaraka vibaya kama anavyofanya Makori,” alisema.
Mafula alisema ni jukumu la kila kiongozi kuheshimu kiongozi mwenzake ili kuweza kufanikisha maendeleo kwa wananchi.
Alisema kosa ambalo aliambiwa amekosa baada ya kukaa polisi kwa saa 48 ni kuwa amezuia wananchi kujiandikisha jambo ambalo si kweli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Kimara Baruti, Kinyonga alisema mkuu wa wilaya ni mbabe na anatumia lugha za kuzalilisha.
Kinyonga alisema anaamini kuwa kupitia tume ya maadili muafaka utapatikana naa itakuwa njia na muongozo sahihi kwa viongozi wengine ambao wanafanya vitendo kama hivyo.
“Mimi nimechaguliwa na wananchi yeye ameteuliwa kitendo cha kutamka mbele ya wapiga kura wangu kuwa ni mpumbavu au mjinga ni kunidhalilisha na kuwatukana hivyo tafsiri sahihi itatolewa na tume,” alisema.
Mwenyekiti wa Makoka, Akyoo alisema aliwekwa ndani ya kituo cha polisi kwa saa zaidi ya 60 bila kuabiwa sababu yoyote.
Alisema katika kutatua changamoto ambazo zinatokea ni vema viongozi wakashirikishana ila mkuu wa wilaya amekuwa akitumia mamlaka yake kuwajibisha viongozi wenzake bila kufuata taaratibu.
Akyoo alisema baada ya uchunguzi alibaini kosa lake lilikuwa ni kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika mchakato wa kugawa maeneo jambo ambalo lilikuwa ni agizo la waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.
Mwenyekiti huyo alisema kilichomsukuma kufika ofisi za maaadili ni kuhakikisha kuwa kumbukumbu zinakuwepo kuhusu matukio hayo ya viongozi.
Akijibu tuhuma hizo Makori alikiri kuchukua hatua hizo za kuagiza wawekwe ndani huku akibainisha kuwa sababu za msingi ni viongozi hao kushindwa kusimamia majukumu yao.
Alisemaa yeye hayupo Ubungo kufanya siasa hivyo walalamikaji hawana hoja na sasa hakuna mchezo kinachohitajika ni kila mtu kufanya kazi.
“Waambie waseme ukweli sababu za kushikiliwa na polisi waache porojo mimi sitaki porojo, mwenyekiti wa kwanza, wapili, watatu, wanne ambao nimewawekwa ndani wanatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), baadae niliwaweka wa Chadema ila hoja za msingi zipo na nitaendelea kuwaweka ili waweze kufuata sheria na kufanya kazi na kuachana na mazoea,” alisema.
Makori alisema wenyeviti hao walikuwa na mambo yao yasiyokubalika Serikalini hivyo waende tume, polisi, kwenye vyombo vya habari au kokote hatarudi nyuma.
Alisema wapo wenyeviti matapeli, wabadhirifu na wanakosa maadili hivyo Serikali ya Ubungo kupitia yeye haiwezi kuvumilia uovu huo.
“Yupo mwenyekiti amepandisha bei ya kupima maeneo kutoka sh. 200,000 hadi 400,000 sasa huyo utamuacha akae mtaani nataka wabadilike,” alisema.M
Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Maadili ya Umma, Joseph Ishengoma amesema hana taarifa rasmi lakini inawezekana viongozi hao wamewasilisha malalamiko ofisini

No comments:
Post a Comment