Makontena yenye samani ofisi za walimu yawasili nchini....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amepokea shehena ya makontena 20 kati ya 36 yenye samani (furniture) zenye thamani ya sh billioni 2 zilizotolewa na Diaspora waishio nchini Marekani wakiunga mkono kampeni ya ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu jijini Dar es salaam.
Ndani ya Kontena hizo zipo meza za umeme zenye hadhi ya kimataifa 2500, meza za kawaida 2500,Viti zaidi ya 5,000,Makabati makubwa ya vitabu 1300, Ubao za kisasa (writing board) zisizotumia chaki 700.
Vifaa hivyo vya kisasa vimetolewa na Jumuiya ya watanzania waishio Marekani ijulikanayo kama Sixth Region Diaspora Caucus Washington.
Akizungumza wakati wa kupokea makontena hayo, Makonda alisema jumla ya kontena zilizotolewa na jumuiya hiyo ni 36 na kati ya hizo 20 zimefika na mengine 16 yapo njiani.
Alisema lengo ni kuboresha mazingira ya walimu na kurejesha heshima yao ili wapate morali ya kufundisha
Aidha ameshukuru Benki ya Walimu kwa kusaidia kulipia usafirishaji wa makontena matatu na kuwaomba wadau kusaidia kulipia gharama za usafiri wa makontena mengine kama mchango wa kutambua thamani ya mwalimu.*

No comments:
Post a Comment