BoT yapiga 'stop' maduka 86 ya kubadilishia fedha...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeyafutia leseni maduka 86 ya
kubadilishia fedha za kigeni baada ya kushindwa kutimiza masharti.
Masharti hayo ni paomoja na kushindwa kutoa vielelezo vinavyoonyesha vyanzo vya
fedha hizo zinazotumika kwenye biashara hiyo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari
waliohudhuria mafunzo ya kuandika habari za kiuchmi mkoani Mtwara meneja wa
kitengo kinachosimamia fedha za kigeni kutoka BoT Eliyamringi Mandari amesema
kufungwa kwa maduka hayo kunatokana na oparesheni inayoendelea nchi nzima kwa
sasa yenye lengo la kuleta ufanisi wa kazi katika maduka hayo.
“Opereresheni hii inakwenda sambamba na
usajili mpya wa maduka haya ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo umetokana na
kanuni mpya ya kuyasimamia, lengo hasa ni kuongeza ufanisi na mitaji katika
kuendesha biashara hii,” amesema Mandari.
Hata hivyo amesema katika
oparasheni hiyo maduka 297 yametuma maombi ya kupatiwa leseni huku 65
yakiendelea kufanyiwa kazi na 71 tayari yamepatiwa leseni mpya pamoja na matawi
yake arobaini.
Mandari amesisitiza kuwa baada ya wiki
mbili zijazo zoezi hilo litakuwa limilika na taarifa kamili itatolewa.
Ameeleza kwamba ni kosa la
jinai kwa mtu yeyote kuendesha biashara ya fedha za kigeni bila leseni ya benki
kuu na adhabu yake ni faini ya sh. milioni 4 ama kifungo cha miaka 14 gerezani
au vyote viwili kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment