Tanzania yaongoza uchumi kusini jangwa la sahara...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam


TANZANIA imetajwa kuongoza katika uchumi jumuishi kusini mwa Jangwa la Sahara huku ikiongoza kwa utawala bora ukanda wa nchi za Afrika Mashariki ikifuatiwa na Kenya.

Pia Tanzania imeingia tano bora katika ukuaji wa uchumi Afrika ikiongozwa na Ghana, Ethiopia, Kodivaa, na Senegali.


Dk Hassan Abass



Msemaji mkuu wa Serikali, Dk.  Hassan Abasi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kwamba pamoja na changamoto za uchumi duniani ripoti mbalimbali zimeendelea kuitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi  zenye uchumi na utawala bora wa kuigwa duniani na Afrika.


"Ripoti ya World Economic Forum(WEF),ya Januari 23,2018 iitwayo 'The Inclusive Development Index, 2018 imetaja Tanzania kuongoza Afrika katika uchumi jumuishi, "amesema.


Amesema Tanzania imekuwa nchi ya pili katika uchumi jumuishi Afrika nzima ikiongozwa na Tunisia ikifuatiwa na Ghana na Kameruni.


Dk Abasi amesema utawala bora ni kigezo muhimu cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa jamii.


"Kwa mujibu wa orodha ya hali ya demokrasia duniani (2017 Democracy Index) iliyozinduliwa Februari 2, 2018 iliyotolewa na 'The Economist Intelligence unit' cha jarida kongwe na mashuhuri duniani la The Economist, Tanzania ni ya kwanza katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki,"amesema.


Amesema dhamira ya rais John Magufuli ni kuhakikisha uchumi mkuu wa unaoendelea kujiakisi katika maisha ya watanzania kupitia utoaji wa huduma mbalimbali za kiuchumi.


Akizungumzia upatikanaji wa maji nchini, Dk. Abasi amesema serikali imekamilisha mirado 10 mikubwa ya maji ya kihistoria.


Amesema usambazaji wa umeme mijini na vijijini, katika kutekeleza mradi wa REA, sh bilioni 985.5 zitatumika kuwafikishia umeme katika mpango maalum iliyoanza kutekelezwa.


Ameongeza kuwa, ujenzi wa barabara za juu Tazara umefikia asilimia 70 na kwamba hadi Oktoba itaanza kutumika.


"Mwaka huu serikali inakusudia kutekeleza upanuzi wa njia za mwendo kasi jijini Dar es Salaam kwenda barabara ya Kilwa Mbagala kwa kilomita 19 na barabara ya uhuru kwenda Gongo la mboto ya kilometa 23.9,"amesema.


Ameongeza  katika kuleta mageuzi katika sekta ya Kilimo, rais ameshasaini sheria ya kuanzisha taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) itakayotoa mfumo mpya wa kisasa wa uuzaji mazao kupitia soko la kimataifa la bidhaa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search