Mashine za EFDs zakosekana Mbeya vijijini...soma habari kamili na matukio360..#share
Na mwandishi wetu, Mbeya.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbeya vijijini, inakabiliwa na changamoto ya
upungufu wa mashine za risiti za kielekroniki(EFDs) na kuchangia kupoteza mapato hususan kwa wafanyabishara kukwepa kulipa ushuru.
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya vijijini wakiwa kwenye kikao cha kupitia taarifa ya bajeti ya mwaka 2017/18 leo katika ukumbi wa halmashauri
baraza la Madiwani wakati akisoma taarifa ya bajeti ya mwaka wa fedha
2016/17 ambapo Sh 42 bilioni zilitumika kwa ajili ya malipo ya posho
za madiwani,mishahara ya watumishi ,uendeshaji wa vikao vya
kisheria,na kutoa mikopo kwa wanawake na vijana na miradi ya maendeleo
Amesema mahitaji ni mashine 160, zilizopo 120 na upungufu 40 na
kwamba kulingana na changamoto hizo mwaka wa fedha 2018/2019 wametenga Sh milioni 14
kununua mashine hizo
Mkuu wa Wilaya Poul Ntinika , aliwataka watumishi wa halmashauri
kushirikiana na madiwani kusimamia kikamilifu vyanzo vya mapato ya
ndani na kudhibiti mianya ya rushwa ili kuondokana na utegemezi wa
fedha kutoka Serikali kuu .
Ntinika amesema uwezo wa halmashauri hiyo kujiendesha ni asilimia 6.7
na kutegemea fedha kutoka serikali kuu zaidi ya Sh bilioni 42 .
Amesema Mbeya ni moja ya mikoa inayotegemewa kwa
chakula nchini hivyo ni jukumu la madiwani katika maeneo yao
kuangalia changamato zinazoguza sekta hiyo.
Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza ameitaka halmashauri hiyo
kusimamia fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya
maendeleo na zisitumike vinginevyo.
"Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi ya maendeleo
hususan katika kilimo sasa ni jukumu letu sote kuelekeza macho ili
kusaidia ukauji wa uchumi kwa kufuatilia miradi hiyo "alisema.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mwalongo Kisemba amesema halmashauri hiyo
inapoteza mapato mengi kutokana na baadhi ya mawakala wanaokusanya
ushuru kutokuwa waaminifu sambasamba na kukosefu wa mashine za EFDs
katika baadhi ya maeneo.



No comments:
Post a Comment