Kesi ya mchungaji Mwingira yafutwa...soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk William Morris raia wa Marekani  dhidi ya mkewe Dk Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira.



Akisoma hukumu leo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dk Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuthibitisha mahusiano ya kimapenzi  kati ya Dk Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa ni matokeo ya  mahusiano ya kimapenzi kati ya Dh Phills na Mchungaji Mwingira.

Hivyo mahakama imeitupilia mbali kesi hiyo ya madai na kusema mdai ameshindwa kuthibitisha kesi hiyo katika kiwango kinachotakiwa katika kesi za madai na alipe gharama za kesi. Pia gharama walizotumia wadaiwa.

Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo wakili Respicius Ishengoma watakata rufaa kwa sababu hawajaridhika na hukumu hiyo.

Hukumu hiyo imeandaliwa katika kurasa 54 imesomwa Leo nyakati za saa 8 mchana, hukumu hiyo imeandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu,Godfrey Mhini na kusomwa na Hakimu Simba.

Awali katika utetezi wa Dk Phills Nyimbi aliieleza mahama hiyo kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.

Akiongozwa na wakili Peter Swai kutoa  ushahidi katika kesi ya madai iliyofunguliwa na aliyekuwa mumewe ambaye ni raia wa Marekani, Dk William Morris, Dk Nyimbi aliomba mwanaume huyo asilipwe kiasi cha fedha cha Sh 7.5 bilioni anazodai Kwa sababu yeye hakuwa na mahusiano na Mchungaji Mwingira.

Dk Nyimbi kupitia Wakili wake Swai aliomba Dk Morris asilipwe kiasi hicho cha fedha Kwa sababu yeye hajawahi kuwa na mahusiano na Mchungaji Mwingira  na kwamba  hicho anachokidai siyo madai halali.
Wakili Swai alimuuliza Dk Nyimbi anasemaje kuhusu madai ya mumewe Dk Morris, kuwa wewe na yeye mkapimwe HIV.

Dk Nyimbi alidai kuwa yeye mwenyewe huwa anautaratibu wa kupima na kwamba Kwa bahati nzuri  sheria za Tanzania zinaruhusu.
Swai alimueleza Dk Phillips kuwa mumewe Dk Morris anataka mtoto wake akapime vinasaba (DNA).

Dk Phillips alidai kuwa mtoto huyo ni wa kwake yeye, Dk Phillis na hajasema ni wa Dk Morris  wala wa Mchungaji Mwingira.
Pia ameiomba Mahakama iamiru gharama za kesi zilipwe na Dk Morris.
Dk Nyimbi  alisisitiza  Kukana  kuzaa na Mchungaji Mwingira na kwamba Mchungaji huyo wala hajawahi kuujua mwili wake.

Dk Nyimbi alitoa utetezi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhini.
Alidai kuwa  alifunga ndoa na Dk Morris mwaka 2001 katika Kanisa la Mtakatifu Albano.
Alieleza kuwa  baada ya ndoa walikaa mapumziko kwa siku tatu katika Hoteli ya Starlight kisha wakahamia Muhimbili ambako alikuwa anaishi katika chumba kimoja akiwa katika mafunzo ya vitendo.

Alidai kuwa baada ya miezi mitatu Dr Morris  alikwenda Marekani na kwamba Mawasiliano kati yao yalikuwa ya shida shida.
Alidai kuwa kutokana na hali hiyo alichanganyikiwa kwa kuwa madaktari wenzake walikuwa wakimuuliza  anaondoka lini na kwamba alikuwa  akilia tu.

Alidai kuwa alijaribu kwenda katika  Ubalozi wa Marekani mara mbili kutafuta Visa ya kusafiria lakini ilishindikana hivyo akaamua kuendelea kusoma ili asije akakosa  vyote.
Alidai kuwa Dk Morris baada ya miaka minane  alikuja Tanzania Aprili 25, 2009  baada ya kupata taarifa anakuja alikwenda  kumpokea katika uwanja wa ndege wa KIA.

Alidai kuwa baada ya kumpokea walilala katika  hoteli iliyopo Moshi ambapo usiku huo alimuelezea historia ya maisha yake, kwa muda mrefu, aliomuacha.
Alimueleza kuwa anamsisha yake amezaa na ana mtoto wa mwaka mmoja. Alimueleza kuwa  alimuoa akiwa na miaka 30 hivyo amezaa akiwa na miaka 38.

Alidai kuwa alimueleza alimsukuma kitandani. Alieleza Dk Nyimbi.
Dk Nyimbi alidai waliporudi nyumbani kwao Kibaha mkoani Pwani alimwambia kwamba mtoto huyo wa kiume kazaa na mfanyabiashara ambaye yuko nje ya nchi anaitwa Baraka.
Alidai Dk Morris alisema ana kuna ili mtoto huyo atakuwa wake kwa sababu anampenda mkewe lakini siku zilivyokuwa zikienda mumewe alimwambia kwamba mtoto huyo kazaa na Nabii Mwingira.

"Aliniambia naitwa Polisi Kibaha nikatoe maelezo kuhusiana na mtoto, nilikataa, nikapigiwa simu na Polisi Kibaha ndipo nilipoamua kwenda, niliambiwa kwamba mu
mewe wangu kalalamika kuwa  nimebakwa na Nabii Mwingira na nimezaa naye mtoto." Alieleza Dk Nyimbi.

Alidai kuwa alipoulizwa na Polisi alikataa kwamba hakuna jambo kama hilo na kwamba hajawahi kubakwa wala kuzaa na Mchungaji Mwingira.

Kwa upande wa Mchungaji Mwingira naye alikana kuwa na mahusiano ya Kimapenzi na Sh Phills.
Katika kesi hiyo, Dk Morris ambaye ni raia wa Marekani pamoja na mambo mengine anaiomba mahakama hiyo imuamuru Mwingira kulipa Sh 7.5 bilioni  kama fidia  ya kuzini na kuwa na mahusiano na mke wake huyo.

Pia anaomba itoe amari ya kwenda kupima Ukimwi  kwa yeye, Mchungaji Mwingira na mkewe Phillis na ifanyike kipimo cha DNA  kati ya mtoto  na walalamikiwa hao.

Inadaiwa kuwa Mwingira na Phillis waliingia katika mahusiano muda usiojulikana bila ya kujali kuwa Phills alikuwa ni mke wa Morris na kwamba mara baada ya Morris kufanya uchunguzi  juu ya mahusiano hayo mke wake alidai kwamba yeye alibakwa na Mchungaji Mwingira.

Iliendelea kudaiwa kuwa kubakwa huko  kulipelekea  siyo tu mke wake  kuwa na ujauzito pia kulisababisha  kuwa na matatizo ya afya.

Desemba 28,2011 Morris na Phills  walifunga  ndoa  ya Kanisani  na wakati wa mahusiano yao, Phillis na Mchungaji Mwingira wanadaiwa  kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na kubahatika kupata  mtoto wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 9.

Mlalamikaji huyo anadai kuwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi  Kibamba  ambapo walimueleza  kuwa suala hilo  ni la uzinzi  ama udhalilishaji  na haliwezi kuwa la kijinai na kushauriwa kufungua  kesi ya madai.

Kitendo cha mke wake kuwa na mahusiano na Mwingira  ni kwenda kinyume  na ndoa yao halali  na kwamba kitendo hicho  kimeharibu mipango yake ya mbele  kiasi cha kumfanya  apoteze hata matumaini ya kuendelea kuishi.

Pia kimemuaibisha na kushusha hadhi yake siyo tu Tanzania  na Duniani hivyo  kumsababisha ateseke kiakili na kiuchumi.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search