Shahidi: Wema anatumia bangi kama starehe....soma habari kamili na matukio360....#share


Na mwandishi wetu, Dar es salaam

SHAHIDI wa tatu wa upande wa mashtaka, WP 6441 DC Mary (35) ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa msanii wa filamu,  Wema Sepetu  alimueleza kuwa anatumia bangi kama starehe.


Wema Sepetu akiwa mahakamani

WP Mary ameeleza hayo leo wakati akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akitoa ushahidi, WPMary alidai kuwa Februari4,2017 alipewa maelekezo na mkuu wake wa kazi OC CID Denis Mujumba kumtoa Wema mahabusu na kwenda nyumbani kwa Wema kufanya upekezi.

Amedai kuwa alimtoa Wema mahabusu na kuondoka naye katika gari wakiwa yeye, OC CID Mujumba, Inspekta Wille, Koplo Robert na DC Hassan kuelekea nyumbani kwa Wema Bunju Basihaya.

Amedai kuwa wakiwa njiani alimueleza Wema kuhusu tuhuma zinazo mkabili kuwa anahusika na uuzaji wa dawa za kulevya ama kutumia.

Shahidi huyo alieleza kuwa baada ya kumueleza Wema hayo, alisema yeye hajishughulishi na uuzaji Ila anatumia bangi kama starehe.

Alidai kuwa alimuuliza Wema kuwa ni lini ilikuwa mara mwisho kutumia bangi  nakwamba siku hiyo ilikuwa Jumamosi ya Februari 4,2017.

Wema alimwambia kuwa  Mara ya mwisho kutumia bangi ilikuwa siku ya Jumatatu.
Alieleza kuwa wakati huo walikuwa njiani na kwamba  walipofika nyumbani kwa Wema waligonga geti na likafunguliwa na mfanyakazi mmoja wa Wema, wakaingia ndani   na kwamba walipoingia walimkuta mfanyakazi mwingine wa Wema.

Alidai kuwa kabla ya upekuzi Wema aliomba Dada yake Nuru Sepetu apigiwe simu ili awepo katika upekuzi, akapigiwaakafika pamoja na mjumbe Steven Ndoho naye aliitwa.
Ushahidi huyo alidai kuwa baada ya watu hao kufika Dada yake Wema,Nuru aliomba kuwapekua kwa sababu wanawea kumuwekea Wema kitu chochote.

Alidai kuwa walianza upekuzi jikoni ambapo walikuta msokoto mmoja wa bangi na Rizla moja kwenye shelfu za kabati.
Walipekuwa sebuleni hawakukuta kitu chochote, katika chumba cha Wema cha kuvalia nguo na viatu walikuta kipisi kimoja cha bangi dirishani.

Pia walipekuwa katika chumba cha wafanyakazi walikuta kipisi kimoja cha bangi ndani ya kiberiti katika droo ya kitanda.
Ushahidi huyo alieleza kuwa baada ya upekuzi huo wote walitoka nje na kuandika maelezo ambapo Afande Wille alijaza hati ya ukamataji mali na wakarejea polisi.

Aliongeza kudai kuwa February 8,2017 saa 4 asubuhi Inspekta Wille alimpatia maelekezo ya kumpeleka Wema kuchukuliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Alidai kuwa baada ya kupewa maelekezo hayo, waliondoka kituoni yeye, Inspekta Wille, Wema na Nuru Hadi kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo Inspekta Wille aliingia kwa Mkemia na kutoka na kikontena cha plastiki kikiwa kimefungwa na kumkabidhi.

WP Mary alieleza kuwa baada ya kukabidhiwa kikontena hicho alielekea chooni ambapo Wema aliingia kutoka sampuli ya mkojo na yeye akabaki mlangoni akimsubiri.
Alidai kuwa baada ya Wema kumkabidhi kikontena kikiwa na maji yenye rangi ya njano naye alimkabidhi Inspekta Wille kwa ajili ya kumkabidhi Mkemia.

Aliendelea kudai baada ya hapo walirudi  Polisi  na akamtambua Wema mahakamani hapo ushahidi huyo. Wafanyakazi wa Wema ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Wakili Albert Msando baada ya ushahidi huyo kutokaushahidi, alimuuliza kati ya mshtakiwa wa pili na wa tatu  ambapo ni wafanyakazi wa Wema alimkamata na bangi.

WP Mary alieleza kuwa hakuna aliyemkamata .
Wakili Msando  unakiri ushahidi wao ni kuhusu upekuzi katika nyumbani ya Wema.
WP Mary ninakiri
Wakili Msando ulihusika mahali popote kuchukua maelezo ya washtakiwa namba mbili na tatu.
WP Mary sikuhusika
Kesi imeahirishwa hadi Machi 12 na 13,2018 ambapo mashahidi wataendelea kutoa ushahidi dhidi ya Wema na wenzake.
Katika kesi hiyo inadaiwa  kuwa  Februari 4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.
Wema ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Februari 3, 2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search