Magufuli asikitishwa kifo mwanafunzi NIT, aagiza hatua za kisheria zichukuliwe....soma habari kamili na matukio360....#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
RAIS John Magufuli ametoa pole kufuatia kifo cha mwanafunzi
Akwilina Akwilini na ameagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika.


Mwanafunzi huyo wa chuo cha usafirishaji Tanzania (NIT) alipigwa risasi akiwa ndani ya daladala jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa majira ya jioni, ikiwa siku moja kabla ya uchaguzi mdogo wa  ubunge jimbo la kinondoni kufanyika.

Ametoa pole hizo kupitia ukarasa wa twita:



Kifo hicho kilifuatia baada ya kuibuka makabiliano kati ya jeshi la polisi na wafuasi wa chama cha Chadema
Walioshuhudia wanasema kuwa maafisa wa polisi walitumia vitoa machozi na risasi katika harakati za kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha Chadema waliokuwa wakiandamana hadi afisi za tume ya uchaguzi.
Baadhi ya wanachama wa chama hicho walikamatwa.Mwili wa msichana huyo ulikuwa na jeraha la risasi kichwani
Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, mwanafunzi huyo alikuwa safarini kulekea Bagamoyo kupeleka fomu za kuomba nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo mjini Bagamoyo.

Akwilina Akwilini

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search