Mamlaka ya maji Mbeya yatimiza lengo...soma habari kamili na matukio360...#share
Na mwandishi wetu, Mbeya.
MAMLAKA ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya(Mbeya-uwsa) imefikia asilimia 100 ya utekeleza agizo la Waziri wa Nchi Ofisi wa Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo ya kuzitaka mamlaka zote kufunga mita kwa wateja ili kuthibiti upotevu wa maji.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji mkoani mbeya, Simion Shauri
Waziri Jafo alitoa agizo hilo, Februari 12 , Mkoani Dodoma wakatI
akipokea ripoti za utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira
za makao makuu,wilaya, na miji midogo na kwamba atazifuta bodi za
mamlaka ambazo zitashindwa kutekeleza agizo kwa asilimia 90 ifikapo
mwezi juni mwaka huu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji, Dkt, Lwitiko Mwakalukwa ameiambia
matukio360 kuwa mamlaka bado inaendelea kutekeleza zoezi la ufungaji
mita za ruku kwa wateja licha ya kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya
wateja kuchakachua mita na wizi wa maji.
"Tumefikia asilimia mia ya utekelezaji wa agizo la Waziri na sasa
tuna mradi mkubwa utakaonganishwa katika mto Kiwila Wilaya ya Rungwe
utakaohudumia wananchi wa Jiji la Mbeya na Mamlama ya mji mdogo wa
Mbalizi na vijiji zitakavyozunguka mradi huo wenye thamani ya Sh bilioni 42
ambao utaanza kutekelezwa hivi karibuni,"amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa (Mbeya-Uwsa) Mhandisi, Simon
Shauri amesema mbali na kuwepo kwa mradi mkubwa wa maji pia
wamejenga jengo la kisasa la ofisi za mamlaka hiyo lenye thamani ya Sh
1.6 Bilioni na sasa limefikia asilimia 75.
Shauri amesema mbali na mafanikio hayo bado kuna changamoto ya
upungufu wa maji kwa asilimi 28 ambao unasababishwa na wizi wa maji
shughuli za kijamii katika vyanzo vya maji na hali ya tabia nchi.
Ofisa habari wa Mamlaka hiyo, Neema Stanton aliitaka jamii
kushirikiana na Mamlaka hiyo kuwafichua watu wanaojihusisha
na uharibifu wa vyanzo vya maji ili kuepukana na majanga yanayoweza
kujitokeza.
About Author Matukio360
Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.
No comments:
Post a Comment