Tetesi za soka Ulaya leo Jumanne....soma habari kamili na matukio360....#share
Na mashirika ya kimataifa
Tottenham ina mpango wa kufanya jitihada mpya kumpata winga wa Crystal Palace, Wilfried Zaha (25). Klabu hiyo ya Mauricio Pochettino ilishindwa baada ya kujaribu mara mbili kumpata mchezaji huyo raia wa Ivory Coast. (Mirror)
Wilfred Zaha
Paris St-Germain hawana nia ya kumsaini mlinzi wa Manchester United Marcos Rojo( 27), licha ya kuhusishwa na mpango wa pauni milioni 30. Pia ni mchezaji wa Argentina. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Real Madrid Marco Asensio, 22, anasema amepata ofa kutoka vilabu vitano vikiwemo Liverpool, Chelsea, Arsenal, Bayern Munich na Juventus, lakini rais wa klabu ya Florentino Perez hataki kumuuza raia huyo wa Uhispania. (Diario Gol - in Spanish)
Ajenti wa Nabil Fekir amekataa kuthibitisha ikiwa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa ambaye amelengwa na Arsenal na kwamba atajiunga na Lyon msimu ujao. (Telefoot via Mirror)
Kiungo wa kati wa Real Madrid na mjerumani Toni Kroos, 28, ni lengo kuu la Manchester United, ikitaka achukue mahala pake Michael Carrick ambaye anastaafu msimu ujao. (Independent)
Alan Pardew anajaribu kuokoa kazi yake huku West Brom na kipigo walichokipata kutoka Huddersfield siku ya Jumapili kinaweza kumaliza kuwepo kwake katika klabu hiyo baada ya wiki 12 tu.
Everton itabaki bila ya mlinzi wa mkopo wa Manchester City, Eliaquim Mangala kwa msimu wote baada ya mlinzi huyo mfaransa kupata jeraha wakati wa ushindi dhidi ya Crystal Palace. (ESPN)
Mshambuliaji wa Argentina Leonardo Ulloa, 31, anasema anataka kuhama kwake kwa mkopo kutoka Leicester kwenda Brighton kuwe wa kudumu mwisho wa msimu. (Argus)
Klabu ya Sunderland imetangazwa kuuzwa kwa pauni milioni 50. (Mirror)
Kylian Mbappe atakamilisha kuhama kwake kwa pauni milioni 166 kutoka Monaco ikimaanisha kuwa PSG watamnunua mchezaji huyo wa miaka 19 raia wa Ufaransa. (Mail)




No comments:
Post a Comment