Serikali kuanza kuweka alama za mipaka ya kimataifa...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Mara
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula amesema Serikali itaanza kuweka alama za mipaka ya kimataifa katika mipaka yake na nchi jirani ya Kenya na Uganda kuanzia machi mwaka huu.
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula amesema Serikali itaanza kuweka alama za mipaka ya kimataifa katika mipaka yake na nchi jirani ya Kenya na Uganda kuanzia machi mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious
Luoga wakiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Kenya wa hifadhi
ya Masai Mara ambayo inapakana na hifadhi ya Serengeti wakati alipokagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime
mkoa wa mara.
Hatua hiyo inafuatia baadhi ya
alama za mipaka yake na nchi jirani katika maeneo mbalimbali kuharibika
ama kuchezewa na hivyo kuleta mkanganyiko baina ya Tanzania na nchi hizo
ni wapi mwisho wa mipaka.
Akizungumza katika ziara yake
mkoani Mara, Mabula amesema kwa sasa fedha kwa ajili ya kazi hiyo imeshatengwa
na kinachosubiriwa ni kuanza rasmi kwa kazi hiyo hapo machi mwaka 2018.
‘’katika zoezi la kuweka alama za
mipaka vitawekwa vigingi kila baada ya umbali wa mita mia moja sambamba na
kubainishwa eneo la ardhi huru’’ alisema Mabula.
Kwa mujibu wa naibu waziri huyo,
tayari timu ya wataalamu kutoka nchi za Kenya Uganda na Tanzania zimeshakutana
na kukubaliana kuhusiana zoezi la uainishaji mipaka ya nchi hizo.
Amesema
kwa sasa alama zitawekwa katika mipaka iliyopo mikoa ya Mara, Arusha,
Kilimanjaro na Tanga na baadaye zoezi litaendelea katika maeneo mengine ya
mipaka.
Amesema, ni imani yake baada ya
kukamilika kwa zoezi la kuweka alama za kimataifa za mipaka suala la migogoro
kuhusiana na mipaka litakwisha.
Kwa mara ya mwisho zoezi la
kuweka alama za mipaka ya kimataifa baina ya Tanzania na nchi jirani
lilifanyika mwaka 1975 baada ya lile la awali la Tangazo la Serikali (GN) mwaka
1965 kuhusiana na mipaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Tarime Grorious Luoga alimueleza naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kuwa, mbali na suala la mipaka ya kimataifa wilaya yake inakabiliwa na
changamoto ya mipaka baina ya hifadhi ya Serengeti na wananchi wanaozunguka
hifadhi hiyo kwani wamekuwa wakivamia na kujenga ndani ya hifadhi na wakati
mwingine kuingiza mifugo.
Katika ziara yake ya kukagua
mpaka wa Tanzania na Kenya katika eneo la Serengeti, Naibu Waziri wa Ardhi,
nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula alifuatana na Mkuu wa Wikaya ya Tarime
Glorious Luoga pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Upimaji Vijijini kutoka Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Huruma Lugalla ambapo kwa pamoja walijionea
hali halisi ya mpaka wa Tanzania na Kenya na baadhi ya alama za mipaka
zilizoharibika
No comments:
Post a Comment