Makalla akagua ujenzi barabara lami ya Isyeye....soma habari kamili na matukio360...#share


Na mwandishi wetu, Mbeya
MKUU wa mkoa was Mbeya, Amos Makalla amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa  barabara kuu hadi kata ya Isyeye yenye urefu wa km 2.3  kwa kiwango cha lami  itakayogharimu  Sh milioni 800 kuhakikisha inakamilika kwa wakati
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla, akikagua mradi wa barabara ya isyesye yenye urefu wa kilometa 2.3 ambao utaghalimu Sh 800 milioni, fedha zilizotolewa na serikali




Akizungumza na matukio360 jana kwenye mkutano wa hadhara mara baada
ya Makalla kuzindua ujenzi wa mradi huo na kusikiliza kero za wananchi.
Yohana Samson alisema; "Tunapongeza jitihada za mkuu wa mkoa ni kipindi kirefu wananchi tunalia na ubovu wa hii barabara ya Isyesye hadi barabara kuu jambo ambalo lilikuwa likikwamisha ukuaji wa shughuli za kiuchumi."

Alisema kupitika vizuri na kwa wakati wote itawezesha shughuli nyingi za
kiuchumi kukua kwa kiasi kikubwa.


Kwa upande wake Makalla amewataka wananchi kushirikiana kikamilifu na
mkandarasi ili mradi ukamilike kwa wakati na wajitahidi kuchangia miradi ya maendeleo.

"Wanasiasa wasubiri 2020 kwa sasa hakuna nafasi kwani ilani ya chama
inaelekeza wananchi kusogezewa huduma muhimi na sio kuleta
propaganda,"alisema  Makalla
Mradi huo unasimamiwa na Wakala wa  Barabara za Mijini na
Vijiji (TARURA) na umelenga  kusogeza huduma muhimu kwa wananchi

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search