Masogange alazwa hukumu kesi yake yasogezwa mbele... soma habari kamili na matukio360...#share


Na Abdulrahim Sadiki, Dar es salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kumsomea hukumu, Agnes Gerald 'Masogange' anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu anaumwa na  amewekewa dripu, hawezi kutembea.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri  baada ya upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga na mshtakiwa mwenyewe kujitetea.



Mapema kesi hiyo iliitwa kwa Hakimu Mashauri na wakili wa Serikali Adolf Mkini alieleza kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya hukumu ila mshtakiwa Masogange anayewakilishwa na wakili Ruben Simwanza hakuwapo.

Hata hivyo mdhamini wa Masogange ambaye hakutaja jina lake alisimama na kuiambia mahakama kuwa Masogange hakufika mahakamani kwa sababu anaumwa na akawasilisha nakala za vyeti vya hospitali mahakamani hapo.

Mdhamini huyo alidai  Masogange amewekewa dripu na hawezi hata kutembea.
Kutokana na hali hiyo wakili wa Serikali Mkini aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya hukumu. Hukumu itasomwa Aprili 3, 2018. Wakili mwingine anayemtetea Masogange ni Nehemiah Nkoko.

Masogange wakati akijitete katika kesi hiyo aliiomba  Mahakama imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.

Masogange  ambaye anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya
aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Akijitetea Masogange alidai  mbali ya uvideo Qeen pia alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo.

Masogange katika kesi hiyo  anadaiwa  kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine). Pia anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search