Wateja benki tano zilizofungiwa sasa kulipwa fedha zao.... soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam 
BODI ya Bima ya Amana (DIB) imetangaza  kuanzia Machi 28, 2018 itaanza kuwalipa fidia ya bima ya amana waliokuwa wateja wa benki tano  zilizotangazwa kufutiwa leseni za kufanya shughuli za kibenki  nchini Januari 4, 2018

Makao makuu ya BoT

Bodi hiyo ambayo imepewa mamlaka na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kuwa mfilisi wa taasisi hizo, imewataka wadaiwa na wadai wa taasisi hizo kujitokeza kuwasilisha vithibitisho vya madai yao na mwisho ni   Aprili 17,  2018.

Wenye amana watakaonufaika na malipo hayo ya fidia ya bima ya amana ni waliokuwa wateja wa Njombe Community Bank Ltd, Meru Community Bank, Covenant Bank for Women in Tanzania Ltd, Efatha Bank Ltd na Kagera Farmers’ Cooperative Bank Ltd, ambazo ziko katika ufilisi ambao watatakiwa kutimiza masharti kadhaa ili kupata malipo yao.

Masharti yaliyotajwa ni pamoja na kutambua mahali na muda wa malipo, ukomo wa malipo ya fidia, madai kwa amana zinazozidi shilingi 1,500,000, na kuwa na vitambulisho stahiki.

NB: Taarifa zaidi zinapatikana katika mtandao wa Benki Kuu: http:/www.bot.go.tzhttps:

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search