Shambulizi afisa balozi wa Syria lamuibua Makonda....soma habari kamili na matukio360...#share

Na mwandishi wetu, Dar es salaam


MKUU wa mkoa wa Dar es salaam ameibuka na kusema hataruhusu watu wachache wachafue taswira ya mkoa huo.



Kauli hiyo ni kufuatia jana mchana afisa Ubalozi wa Syria kushambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha Jijini Dar Es Salaam

Picha ya afisa balozi wa Syria aliyeshambuliwa


TAARIFA YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA.

Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha jana mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi.

Nawaomba sana wananchi wa Dar Es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana.

Vyombo vya usalama vinalifanyia kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani.

Tunafuatilia zaidi kujua kwa nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.

Kwa hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.

Uchunguzi ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.

Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search