Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano... soma habari kamili na matukio360...#share
Na mashirika ya kimataifa
Liverpool imesema kuwa haitamuuza mshambuliaji wake Mohamed Salah, 25, mwisho wa msimu huu na kwamba mchezaji huyo wa Misri na kwamba hakuna kipengele katika mkataba kinachomruhusu kuondoka katika klabu hiyo wakati wowote. (ESPN)
Mohamed Salah
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anasema kuwa kujiamini ndio ufunguo wa ufanisi .Mchezaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33 amefunga mbao 21 katika mechi 13 tangu kuanza kwa msimu wa 2018.2018. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure hakushiriki katika mazoezi ya kwanza na timu ya taifa ya Ivory Coast siku ya Jumanne . (Fifciv.com)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 26, amepinga uvumi kwamba anatakakujiunga na PSG kwa kusema kwamba anahisi kuwa nyumbani Stamford Bridge.(Express)
Mchezaji anayelengwa na klabu ya Manchester United, Milan Skriniar, 23, anasema kuwa anafurahia kusalia Inter Milan. Raia huyo wa Slovakia pia ameivutia Barcelona. (star)
Ajenti wa mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial, 22, hajatoa hakikisho lolote kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kusalia katika klabu hiyo. (Il Bianconero, via Independent)
Tottenham imejiandaa kumpoteza beki wa ubelgiji Toby Alderweireld, 29, mwisho wa msimu huu lakini watahitaji kulipwa dau la Yuro 50m (£44m). (HLN - in Dutch)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amewapatia wachezaji wake ambao hawajiungi na timu zao za kimataifa likizo ya wiki moja huku akiwapeleka ,wasaidizi wake wa ukufunzi Tenerife. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic huenda akaingia matatani na shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) kwa kujihusisha na kampuni nyingine ya kucheza kamari.. (Mirror)
Kampuni ya Vodafone nchini Misri itatoa salio la kupiga simu kwa wateja wake wote kila baada ya mshambuliaji wa Liverpool Mohamed salah kufunga bao. (mirror)
Chelsea inaongoza katika kumnyatia beki wa Ujingereza na Man United Luke Shaw, ambaye alikuwa shabiki mkubwa Chelsea akiwa utotoni mwake , iwapo ataamua kuondoka manchester United mwisho wa msimu huu. (Mail)
Maafisa wakuu was klabu ya Manchester United wanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu tabia ya Mourinho dhidi ya Shaw na hatua hiyo huenda ikaathiri thamania ya uhamisho wa mchezaji huyo (Telegraph)
Tottenham iko tayari kurudi Crystal Palace na dau la £40m kumsajili winga Wilfried Zaha, 25, lakini Crystal Palace inaamini kwamba mchezaji huyo ana thamania ya juu zaidi
Liverpool bado haijwasiliana na kipa wa Roma Alisson, 25, lakini raia huyo wa Brazil hayuko tayari kutia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Itali. (Sun)
No comments:
Post a Comment