Bulaya awekwa mahabusu...soma habari kamili na matukio360...#share
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MMWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk. Vincent Mashinji wameondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi central baada ya kuripoti, huku Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ikidaiwa atalala mahabusu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Ester Bulaya
Wengine waliondoka kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Mashinji amesema kuwa wameripoti kituoni hapo kama walivyoamriwa na mahakama, lakini wameambiwa Mbunge Bulaya atabaki mahabusu kwa ajili ya upelelezi.
“Mbunge Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu,” -Dk.Mashinji.




No comments:
Post a Comment