TFF yasikiliza rufaa ya Wambura...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

HATIMYE rufaa inayomhusu aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Richard Wambura, imesikilizwa jana kwa pande zote mbili kukutana katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaa.
Michael Wambura

Kwa mujibu wa Wakili wa Wambura,Emmanuel Muga, amesema pande zote mbili zimemaliza vizuri kikao hicho na mambo yamekwenda sawia, kinachosubiriwa tu sasa ni maamuzi ya Kamati ya Maadili kutoa hukumu.

Muga ambaye anamtetea Wambura, ameeleza TFF wamesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo.

Wambura alikata rufaa kupinga kufungiwa kujihusisha na soka baada ya TFF kumfungia kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine.

Kamati ya Maadili itakaa na kuandaa rasmi na majibu ya hukumu juu ya rufaa hiyo iliyosikilizwa jana Jumamo

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search