Mkurugenzi MNM anyimwa dhamana...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Iringa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi, Iringa, imemnyima dhamana Mkurugenzi wa Kampuni ya MNM, Engineering Service Ltd, Mhandisi Godwin Mshana, kwa tuhuma za kujenga ukumbi wa Chuo Kikuu Mkwawa, (MUCE) chini ya kiwango.

Mshana alifikishwa leo Mei 10, Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, Iringa, David Ngunyale.

Wakili wa Serikali, Blandina Mnyamba amemsomea mashtaka Mshana na kusema kuwa alitenda makosa hayo kati ya 2010 na 2012.

 Amesomewa mashtaka ya kughushi nyaraka za serikali, kujipatia fedha Sh 3 bilioni kinyume na utaratibu na shtaka la tatu ni kuhujumu uchumi katika matumizi ya Sh 2bilioni.

Dhamana ya Mshana imezuiwa na kesi hiyo itasikilizwa tena Mei 22 mwaka huu.

 Mei 2 mwaka huu, akiwa katika ziara Chuo Kikuu cha Muce, Iringa, Rais Magufuli aliagiza uchunguzi ufanyike katika ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa chuo hicho, uliogharimu Sh 8 bilioni.

Pia, Rais Magufuli  aliagiza, aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Philemon Mushi naye ahojiwe kuhusiana na ujenzi huo.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search