Aliyeiba mahindi yakang'ang'ania kichwani apandishwa kizimbani...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKAZI wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Frank Joseph amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mlandizi mkoani Pwani akishtakiwa kwa wizi wa mahindi.

Joseph ambaye tukio la kukamatwa kwake liliibua hisia na mijadala mitandaoni ikidaiwa alishindwa kutua mzigo aliodaiwa kuuiba, alisomewa shtaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Nabwike Mbaba. 

Mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 124/2018 akidaiwa kuiba mahindi debe moja yenye thamani ya Sh20,000. Baada ya kusomewa shtaka, mshtakiwa huyo alikiri kutenda kosa.

Hakimu Nabwike aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 10 ili kupata maelezo ya mlalamikaji ambaye hakuwepo mahakamani.

Licha ya mahakama kumweleza mshtakiwa kuwa dhamana iko wazi na kumpa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh500,000, alishindwa kutimiza sharti hilo hivyo alipelekwa rumande. 

Tangu Mei 3, Joseph alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani Pwani akituhumiwa kuiba mahindi kwa mkazi wa Mlandizi.

Tukio la wizi huo lilivuta hisia kwa jamii baada ya mshtakiwa huyo kudaiwa kushindwa kutua mzigo uliokuwa begani hadi alipokimbilia polisi na mwenye mali kupigiwa simu, ambapo alifika na ‘kumsaidia’ kuutua.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search