Tanzania yashika nafasi ya 7 kuvutia wawekezaji Afrika...soma habari kamili na matukio360...#share
Na
Abraham Ntambara, Dar es Salaam
KITUO
cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema Tanzania imeendelea kushika nafasi nzuri ya
kuvutia uwekezaji katika nchi za Afrika ambapo kwa mwaka jana 2017 imeshika
nafasi ya saba kati ya nchi 10 za Afrika zenye ushawishi wa kuwavutia wawekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe, amesema hatua hiyo ni kubwa
kutokana na akuendelea kupanda kutoka nafasi ya 11 mwaka 2014 hadi nafasi ya 9
mwaka 2016.
“Na
hii naomba sana kusisitiza mwekezaji asiende kutafuta huduma kwenye taasisi
zingine za serikali aje TIC atapata huduma zote ambazo anazihitaji kutoka TIC,
kwa sababu tunao maafisa wa hizo taasisi zingine ndani ya TIC,” amesema Mwambe.
“Sasa
kuonesha kwamba tumedhamilia kuwafikia wananchi lakini pia na wawekezaji
wakiwemo watanzania mpaka kukamilika kwa utekelezaji wake ambao unakuwa ni
miaka kuanzia sasa huwa tunatoa miaka mitatu,” ameongeza.
Aidha amesema kuwa katika kipindi cha miezi minne kituo kimefanikisha kuandikisha miradi mipya 109 inayotarajia kutengeneza fursa za ajira kwa vijana 18,172.
Mwambe
ameongeza kwamba thamani ya miradi hiyo iliyosajiliwa kama itatekelezwa kama ilivyokusudiwa itagharimu Dolla za Kimarekani milioni 13, 342.21.
“Kama
mnavyofahamu ni kwamba mwitikio mkubwa ni waviwanda kwa hiyo bado eneo la
viwanda limeweza kutoa uwekezaji mwingi zaidi,” amesema .
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji wa kituo hicho
John Mnali amesema miundombinu kama umeme na barabara ni changamoto kwa
wawekezaji hivyo serikali inaendelea kulishughulikia na kuboresha mazingira ya
uwekezaji ili uendelee kuongezeka siku hadi siku.
“Kuna
miradi kadhaa ya serikali ambayo inaendelea kwa upende wa Tanesco ya kuweza
kuzalisha umeme na kuhakikisha kwamba umeme unaozalishwa unakidhi mahitaji ya
wawekezaji,” amesema Mnali.
“Na
kama mnavyoona ongezeko la miradi inayoingia imekuwa mingi zaidi ukilinganisha
na mahitaji ya umeme, yaani ukilinganisha na umeme uliopo, kwa hiyo kunakuwa na
umuhimu wakuwa na miradi mikubwa ya umeme ili uzalishaji huo wa umeme uweze
kukidhi mahitaji yote ya wawekezaji wa sasa na wale wanaotarajia kuja,”
ameongeza.
Amewataka
wawekezaji wandani na nje wanaokusudia kuwekeza miradi yao nchini wawekeze
kwani changamoto hizo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment