Serikali yapiga marufuku uuzaji wa mazao shambani...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imewapiga marufuku wafanyabiashara, walanguzi na wakulima kuuza mazao yakiwa bado shambani na kusema pindi atakaebainika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa na kusema kuwa ili kutatua tatizo hilo serikali inaanda mfumo maalumu ambao utatumika katika kuuza mazao kwa soko huria ili kuepusha hasara kwa wakulima.

"Uimarishwaji wa vyama vya msingi vya ushirika na vyama vikuu vya ushirika ili kupitia vyama hivyo wakulima waweze kuuza mazao yao na kujihakikisha soko la mavuno yao. Serikali itasimamia uzwaji wa mazao ya wakulima kwa njia ya minada ili kuweka kuweka ushindani wa bei na kumuwezesha mkulima kupata bei kubwa kama ilivyo katika zao la korosho", amesema Dkt. Mwanjelwa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search