Ugonjwa wapiga kalenda kesi ya Mbunge Chadema...soma habari kamili na matukio360...#share

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Morogoro imeahirisha kesi ya tuhuma za kuchoma ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Sofi baada ya mshtakiwa wa kwanza, Suzan Kiwanga mbunge kwa tiketi ya Chadema kuugua ghafla.

Kabla ya kuhairishwa kwa kesi hiyo leo Alhamisi Mei 17, 2018, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali,  Sunday Hyera ulionekana kutokubaliana na taarifa hizo za ugonjwa.

Hali hiyo ilimfanya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Ivan Msack kumtaka mdhamini pamoja na wakili wa upande wa utetezi, Barthelomew Tarimo kuwasilisha taarifa ya daktari itakayothibitisha taarifa hizo za ugonjwa.

Wakili Tarimo na mdhamini wa Kiwanga walitoka na kwenda kuchukua taarifa hiyo ya daktari wa kituo cha afya cha Aga khan iliyoeleza kuwa Kiwanga anasumbuliwa na kichwa na maumivu ya mwili na kuiwasilisha mahakamani.

Katika taarifa hiyo ya daktari ilieleza kuwa Kiwanga amepumzishwa kwa saa sita na hivyo Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Mei 18 mwaka huu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search