FUATILIA KAULI YA #NAPE ILIYOMUIBUA #POLEPOLE; ASEMA #NAPE AMEKENGEUKA !!
![]() |
| Katibu wa Itikadi na Uenezi (KIU) wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa Mwananchi Communications Limited (MCL) |
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey
Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa
kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni.
Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya
Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la
Mawaziri.
Nape ambayae miongoni mwa #MATUKIO yaliyogubika mkutano huo lilikuwa lile la kuonyeshewa bastola na mtu asiefahamika undani wake kabla ya mkutano wake huo na waandishi wa habari alikuwa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Miongoni mwa kauli zilizoibua hisia mbele ya waandishi Nape alisema: “wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa
wanakunywa bia baa.. nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa
chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna
atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta
kwenye shimo inakwenda,”
Lakini Polepole, ambaye alitembelea ofisi za kampuni ya
Mcl inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The
Citizen na Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa
amekengeuka.
“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati
anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji Polepole, - Mcl online




No comments:
Post a Comment