#NAJUA WAJUA, JEE ULILIJUA HILI LA #FIRST LADY# MTARAJIWA WA NCHINI UFARANSA ? SOGEA KARIBU NIKUJUZE ZAIDI

Bibi na Bwana Marcon
Wakati #Emmanuel #Macron akishinda katika duru ya kwanza ya ya uchaguzi nchini Ufaransa,  mkewe...  Amekuwa kivutio kikubwa katika mitandao ya kijamii, ndani na nje ya nchi hiyo. 

Unajua ni kwanini amekuwa kivutio? Jibu ni kwamba First lady huyu mtarajiwa wa nchi moja tajiri sana kwa viwanda duniani alikutana na Macron wake kipindi tayari akiwa mama wa 39 na watoto watatu(3) wakati Macron mwenyewe akiwa kinda wa miaka 15 tu.

Wapenzi hawa wameweza kudumu wakiwa pamoja kama mke na mume miaka nenda rudi licha ya changamoto kubwa za tofauti ya umri wao mpaka sasa wakati mwana mama huyu anatarajia kuingia Ikulu akiwa na umri mkubwa wa miaka 64,  huku mume akiwa kijana mbichi anaechipukia akiwa na miaka 39 tu. 
Bwana na Bibi Macron katika moja ya #Matukio
Macron  alikuwa  mwanafunzi wa bibi huyo,  ambaye anatarajiwa kuwa miongoni mwa mabibi wa Ikulu(#First Ladies) mwenye umri mkubwa zaidi na umri wake huo wa miaka 64. 

Kuna msemo wa kiswahili husema #age is just number..

Leo bibi Macron ni mke wa Rais na (#First Lady) mtarajiwa...... Mnaonaje hii?

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search