#Emmanuel Macron aibuka kidedea Uchaguzi Mkuu Ufaransa ! amuacha mbali mpinzani wake
MGOMBEA huru wa Urais nchini Ufaransa, Emmanuel
Macron, (39), anakuwa rais wa kwanza kijana katika historia ya nchi hiyo,
kufuatia ushindi wake baada ya kujipatia asilimia 66.06 ya kura zote
zilizopigwa dhidi ya asilimia 33.94 alizopata mgombea wa chama cha National
Front, Bi Marine Le Pen (48).
Bw. Macron ambaye miaka mitatu iliyopita hakuwa
akijulikana miongoni mwa Wafaransa wengi ameshinda katika uchaguzi huo wa awamu
ya pili uliofanyika Jumapili Mei 7, 2017.
Shamra shamra, kelele na vifijo vililipuka miongoni
mwa wafuasi wake ambapo katika hotuba yake, Rais huyo kijana alisema jukumu
lake kubwa ni kuliunganisha taifa la Ufaransa ambalo liligawanyika, na kwamba
dunia nzima ilikuwa ikifuatilia kwa karinbu uchaguzi huo na wakitusubiri sisi
kulinda nuru ya taifa lililokuwa kwenye kitisho kutoka maeneo mengi.
Pamoja na kushindwa kwenye uchaguzi huo, kura
alizopata Bi Le Pen zimedhihirisha ushindi wa kihistoria kwa makundi ya kutetea
haki nchini Ufaransa.
Katika hotuba yake ya kukubali matokeo, Bi. Le Pen
alisema yeye alikuwa kiongozi wa “jeshi” kubwa la upinzani na kuapa kukifanyia
mabadiliko makubwa chama chake.
Hata hivyo idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo
kupindukia katika historia ya chaguzi nchini humo kwa miaka 40 iliyopita.
Habari ya awali
Mgombea Urais kijana nchini Ufaransa, Emmanuel
Macron,(39) ameshinda kwenye uchaguzi wa urais wa nchi hiyo wa mkondo wa pili
uliofanyika Jumapili Mei 7, 2017. Kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa,
Macron amembwaga mwanamama Marine Le Pen baada ya kujipatia asilimia
66.06% ya kura zote zilizopigwa dhidi ya asilimia 33.94, alizopata Bi. Le Pen
kutoka chama cha National Front. (AN).
No comments:
Post a Comment