Aveva ampaisha Billionaire wa Forbes kwa mkwanja mrefu Simba.. asema kamwaga Shs. 125 Million kwa wachezaji.. #share

Rais wa Simba, Evans Aveva amemtangaza mwanachama na mfadhili wa timu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ kuwa shujaa wa klabu hiyo kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa msimu uliopita kwa wachezaji wa timu hiyo na kuiwezesha kupata mafanikio hayo iliyopata.
Alisema, katika msimu huo, Mo aliwapatia wachezaji kiasi cha Sh milioni 125 kwa ajili ya kuwahamasisha kufanya vizuri uwanjani katika mechi zote za ligi kuu na Kombe la FA walizocheza.
Aliyasema hayo katika hafla ya kutoa tuzo kwa wachezaji wake waliofanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu Bara pamoja na Kombe la FA msimu uliopita, ikiwa ni pamoja na kuwapongeza wadau wote waliojitoa kwa mafanikio ya klabu.
“Mo alifanya kazi kubwa sana, kwa hiyo tunampongeza kwa hilo na tumemzawadia cheti kutokana na kuutambua mchango wake ndani ya Simba.
“Lakini pia tunawapongeza wanachama, wapenzi pamoja na mashabiki wetu ambao pia walijitolea michango yao kwa ajili ya kuwahamasisha wachezaji kupambana vilivyo uwanjani ambapo nao kwa upande wao waliweza kuchangia kiasi cha Sh milioni 125,” alisema Aveva.
Katika hatua nyingine beki wa kushoto wa timu hiyo, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ alitangazwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo wa msimu uliopita na kuzawadiwa kitita cha Sh 1,000,000 ambazo alizigawa kwa wachezaji wenzake akisema kwa unyenyekevu kuwa hakucheza peke yake uwanjani.
Hivi karibuni pia, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimtangaza Tshabalala kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kutunukiwa kitita cha Sh milioni 10.
No comments:
Post a Comment